
Hadith #1003
Swahili (Kiswahili)Sayyiduna Abu Qatadha (RadiyAllahu Anhu) anasema: Mtume wa Allah (SallAllahu Alaihi Wa Sallam) aliulizwa, kwa nini unafunga kila Jumatatu? Akasema: Siku ya Jumatatu ndiyo niliyozaliwa na pia siku ya Jumatatu ndiyo niliyopokea wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah (Mtukufu Aliyetukuka).
Reference: صحيح مسلم، كتاب الصيام، باب استحباب صيام ثلاثة أيام۔۔۔الخ، الحدیث 1162