
Hadith #1002
Swahili (Kiswahili)Mtume wetu mpendwa ﷺ Jina la Mtume wetu mpendwa ni Sayyidina Muhammad ﷺ. Mtume wetu mpendwa ﷺ alizaliwa mji wa Makkah Mukarramah, mji maarufu Arabuni. Mtume wetu mpendwa ﷺ alizaliwa mwezi 12 Mfungo 6 (Rabi ul Awwal). Mtume wetu mpendwa ﷺ alizaliwa siku ya Jumatatu, Jina la baba wa Mtume wetu mpendwa ﷺ ni Sayyidina Abdullah Radhi za Allah ziwe juu yake. Jina la mama wa Mtume wetu mpendwa ﷺ ni Sayyidah Aaminah Radhi za Allah ziwe juu yake. Rawdha (Kaburi) Tukufu la Mtume wetu mpendwa ﷺ lipo mji Mtukufu wa Madina. Umri wa Mtume wetu mpendwa ﷺ ulikuwa miaka 63.